Pages

Saturday 19 November 2011

Shambulio la nyuki/manyigu

Nyuki ni tisho kubwa kwa watu ambao ni lazima wafanye kazi nje: wakulima, wafanyakazi wa ujenzi, askari wa doria, na hata wacheza mpira au teseme kila mtu, Nyuki huwa wakali wanapo chokozwa na hwachagui ni nani aliye wachokoza. Nyuki aliye kasirika utamsikia sauti yake ya kuzuzizima na mara nyingi huja kichwani na usoni. Ukiwa katika hali hii jaribu kujikinga kwa kujifunika uso hasa kwa kupandisha shati lako… sorry kwa kina dada!. Vinginevyo kimbia; mwendo kasi wa nyuki unakadiriwa kuwa 19-24km kwa saa hivi ni rahisi kumshinda.
  • Usijaribu kuwapunga kwa kitabu, kitambaa au kitu chochote kufanya hivyo ni kuwapambisha moto
  • Usikimbilie ndani ya mto ziwa, bwawa au pool
  • Usijikinge uso wako kwa mikono kwani haisaidii
  • Kimbia kwa muundo wa zig-zag
  • Kama upo karibu ya nyumba au gari ingia haraka
Baada ya kurupushani hii na matokeo yake umeumwa basi fanya ifuatavyo:
  •  Ondoa ‘mkuki wa nyuki’ kwa kutumia kucha credit card au kisu
  • Usijikune
  • Jipake siki pale ulipoumwa kwa kutumia pamba au kitambaa safi ; kumbuka sumu ya nyuki ni acid kwa hiyo tumia alkaline kusawazisha sumu ya manyigu ni alikaline tumia acid kusawazisha
  • paka papai, kitunguu, kitunguu swaumu pale ulipo umwa ili kupunguza uvimbe.














Friday 18 November 2011

Hangover

Kwa kifupi pombe ni sumu. Wakati unaingiza sumu mwilini mwako, mwili utapatwa na mtiso uliosababishwa na pomba kam matokeo ya sumu hiyo kutembea mwilini mwako. Hangover ni neno mwavuli ambalo linajaribu kukueleza kitu gani umeufanyia mwili huo. Mara kwa mara dalili ni pamoja na maumivu ya kichwa uchovu, na upungufu wa maji mwilini.

OK kabla ya ‘kuyatimba maji’ zingatia:
☺ Kula hasa chakula chenye mafuta kama nyama nk
☺ Kunywa maziwa
☺ Kunywa vijiko 2 vya mafuta ya olive
☺ Meza vidonge vya vitamin
☺ Jihari usichanganye pombe


Tiba:
Dawa ya kwanza kama unafanya kazi piga simu kazini kwako na uwaambie boss kuwa unaharisha sana na kasha pata usingizi wa kutosha.
Mara tu utakapoamka pata glass mbili za maji baridi kasha kikombe kidogo cha kahawa kwa kuwa kahawa inasaidia kurudisha mishipi ya damu iliyovimba katika hali yake ya kaida jihadhari usinywe.
Kunywa juisi ya kutosha hasa juisi ya madaransi, nyanya au machungwa glasi kubwa inatosha
Jihadhari na kunywa kahawa kwa sababu caffeine siyo mzuri kwa hali hiyo
Kunywa KUDZU ni dawa ya kienyeji ya Kichina kama kifungua kinywa. Kinywaji hiki kinaweza kupatikana katika maduka ya chakula kwa afya.
Ukipata nafuu kunywa supu hasa ya kuku itasaidia kurudisha potassium uliyopoteza.
Milkshake ya ndizi; changanya nusu kikombe cha maziwa ndizi mbivu pamoja na asali vijiko vya chai 2.

Fuga Nyuki Kirahisi

Ufugaji wa nyuki ni shughuli muhimu inayosaidia jamii kujipatia mapato ya ziada ili kuboresha maisha yao.
Ufugaji wa nyuki ni mfumo wa kilimo unaohimili na wenye manufaa kwa mazingira.Ufugaji wa nyuki huwapatia watu walio ndani ya umaskini mapato ya ziada ya mara kwa mara,husaidia mazingira na huwa na manufaa mengine:
1. Ni ghali.Watu binaafsi ama mashirika ya kibinafsi kama makanisa,makundi ya wanawake,makundi ya vijanasna vyama vya mashirika vinaweza kuanza na kiasi kiodogo cha pesa.
2. Haihitaji ulishaji wa jumla wa nyuki kwani nyuki hujitafutia chakula chao kwa mwaka mzima.
3. Mizinga inaweza kutengenezwa na mafundi wa humu nchini ingawaje baadhi ya vifaa vinafaa kuagizwa kutoka ng’ambo.
4. Haihitaji ardhi,kwa hivyo wale wenye rasilmali chache wanaweza kushiriki.

Kumbuka katika mikakati ya mradi wa ufugaji wa nyuki moja ni kupata ufahamu wa uhusiano baina ya nyuki na mwanadamu katika eneo lako. Zungumza na wale wanaojihusisha na nyuki. Andamana nao wakifanya kazi na nyuki.
• Ikiwa hauna ujuzi wa kufanya kazi na nyuki,kuna uwezekano wa kujifunza mengi kutoka kwa wafugaji wa nyuki katika eneo lako.Kwa kufahamu jinsi wanavyofanya kazi,unaweza kutoa maoni ya kuboresha kwa kustahilika,na itakuwa rahisi kutumia teknolojia ya ufugaji wa nyuki inayofaa katika eneo lako.
• Pia ,unafaa kupitia visa kadhaa vya kung’atwa kabla ya kujitolea kufuga nyuki.Kung’atwa na nyuki ni sehemu muhimu katika ufugaji wa nyuki.Mfugaji wa nyuki anapaswa kukabiliana nayo.
• Pindi tu unapoelewa uhusiano baina ya nyuki wa kienyeji na mwanadamu,mawazo ya kuanzisha utaratibiu ulioboreshwa unaweza kuundwa.Yafuatwayo ni maswali yanayofaa kutiliwa maanani:
1.Ni nani wa kufanya kazi naye?
2.Vifaa gani vinafaa kutumiwa?
3.Ni wapi pa kuuza bidhaa za mzinga?

Hatua
• Ikiwa ndio unaanza ufugaji nyuki itakuwa bora ikiwa unafanya kazi na mtu mmoja ama wawili katika eneo lako.Kwa kuchagua wakulima wanaoheshimika na uhusiano mzuri na jamii ,juhudi zako zitaongezeka maradufu.Ukifuga nyuki mwenyewe na kutumia utaratibu tofauti na ule unaotumiwa katika sehemu yako
• Ni hatua katika mwelekeo unaofaa. Habari zitasambaa na punde ama baadaye utakuwa ukizungumza na marafiki ama majirani zako kuhusu ufugaji wa nyuki.
• Mara kwa mara anza ufugaji wa nyuki anza na angalau mizinga miwili. Hii itakupatia fursa kulinganisha maendeleo baina ya mizinga, la muhimu zaidi, inaruhusu mradi kuendelea ikiwa koloni moja itaangamia.
• Mabadiiliko huchukua muda. Ni lazima kuanza na wazo. Utoaji wa kufanikiwa wa wazo ni matarajio yanayoweza kutimilika ili kuanzisha utaratibu bora kwa uhusiano baina ya nyuki na binadamu katika maeneo mengine.
• Katika kupanga mradi,weka malengo yanayoweza kutimilika. Mradi mdogo,unaofaulu, una maana kuliko mkubwa uliojaribiwa na haukufaulu.
• Vifaa vitakavyotumiwa kwenye mradi hutugemea hali iliyoko.Unafaa kutathmini uwepo wa vifaa vinavyohitajika vile vile pia msaada wa kiufundi uliopo katika kuchagua aina ya ama aina za vifaa vya mzinga vinavyofaa.
• Tambua watu katika sehemu yako wanaoweza kutengeneza vifaa vya ufugaji wa nyuki ujenzi wake unaweza kuwa mafanikio kivyake.Inawza kuhitaji uvimilivu unaporatibu kupata vifaa pamoja.
• Milango ya uuzaji iliyopo kwa bidhaa za mzinga katika maeneo mengi.Tafuta watu ambao tayari wanatumia asali ama nta ya nyuki. Mara kwa maara wana hamu ya usambazaji thabiti wa bidhaa za hali ya juu. Ikiwa hawatumii asali, waoka mikate na watengenezaji wa peremende wana uwezekano wa kutoa soko.Watafute pia wale ambao wanaweza kutoa soko kwa nta ya nyuki.
Vifaa:
1. Eneo lenye miti pamoja na mauwa
2. Kitengeneza moshi
3. Mizinga iliyo na:
• Kifuniko cha juu ama paa
• Kifuniko cha ndani
• Chumba cha asali
• Chumba cha uzazi
• Ubao wa chini


A Mzinga
B Kifuniko na vile vile sega la asali litajengwa hapo





Unaweza kupata ushauri na maelezo zaidi juu ya Ufugaji na maelekezo ya wapi utapata pembejeo kupitia watu wafuatao:

- Dr. Mushtaq Osman-UDSM
- Dr. Danstan Kabialo-Afri Honey/Tanzania Honey Council
- Mr. Sosthenes Sambua-TPSF
- Mr. David Kamala-Tanzania National Beekeeping Supply Ltd
- Mr. Jumanne Msuya-MNRT Beekeeping Division

Harufu ya Mdomo

Kama kuna kitu kinacho dhalilisha mtu basi harufu ya mdomo ni namba wani.
Unaweza kupiga mswaki meno yako kwa nguvu zote, kugwangua ulimi wako, floss na kusuuza kwa mouthwash na bado pumzi yenye harufu kali anakuja kutoka nyuma ya koo lako. anaerobic bacteria wanaoishi juu ya uso wa ulimi, ndani ya mdomo na katika umio wako ni chanzo cha pumzi mbaya. Kuwepo kwa bakteria hawa kunasababishwa na kuambukizwa na sababu nyingine.
Pamoja na sababu mbali mabali zisabishwazo na tatizo hili hebu tuangalie jinsi gani unaweza kujuwa kama unatoa harufu mbaya ya mdomo? Jaribu:
1. Kuuliza wenzako kama wanahisi harufu mbaya ya mdomo wakati ukiongea
2. Kama unaogopa basi muulize wife au GF
3. Rahisi kabisa kwa wale wenye uwezo wa kunusa ramba kwenye kiwiko cha mkono(pale kiganja na mkono vinapokutana), ngoja kwa muda wa sekunde 2 kisha nusa! Unaona je? Basi hivyo ndivyo wenzako wanavyo ipata harufu yako.

Tiba:
Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku, ni muhimu kupiga mswaki kila baada ya kula ongeza mafuta ya tee tree kwenye dawa ya mswaki au unga wa karafuu. Tumia vijiti vya meno toothpick, floosy au chelewa ya mnazi kuchokonowa meno ili kuondoa mabaki ya chakula. jaribu kukwangua ulimi kutumia mswaki au kijiko. Njia nyingine ni sukutua mdomo kila baada ya kula hii itasaidia kuondoa mabaki ya chakula.
Kuwa na kipande cha karafuu mfukoni kila uendako, uma kidogo na tafuna kila baada ya muda usikiapo kuwa ulimi ni mchachu. Jaribu kupumua kutumia mdomo, hii husaidia mdomo kuwa fresh. Tumia meno yako kusugua meno yako hii husaidia pia kufanya mdomo wako kusababisha mate ambayo yatatumika kumeza bakteria walio mdomoni. Kula machungwa mara kwa mara. Kunywa kijiko kimoja cha apple cider vinegar (siki) kabla ya kula hii inasaidi kuharakisha uyeyushaji wa chakula na kuondoa harufu mbaya.
Mwisho tengeneza chai ya karafuu; chukuwa karafuu robo kijiko cha chai changanya na vikombe 2 vya maji moto kisha sukutuwa mdomo wako mara kwa mara.

Namna ya kupima Sidiria

Kina mama wengi wamekuwa wakivaa sidiria (Bra) ambazo si saizi yao! Hali hii hupoteza faraja na hata usalama kwa mvaaji hasa wale wenye matiti makubwa. Ukubwa wa matiti hubadilika mara kwa mara sababu muhimu ya mabadiliko haya ni ujauzito na baada ya kujifungua, au wakati mwingi kuongezeka au kupungua kwa ujazo wa mwili. Inashauriwa kujipima au kujaribu sidiria tofauti kila baada ya miaka miwili. Baadhi ya maduka hutoa huduma ya kupima saizi ya Sidiria lakini ni vizuri kama utakuwa na ufahamu wa namna gani unaweza kujipima mwenyewe. Zifuatazo ni hatua za namna ya kupima ili kujuwa ni sidiria kiasi gani ita kufaa.

Kwanza tujuwe misamiati; kuna BAND na CUP muhimu hapa ni kwamba band ni ukubwa wa kufua mfano 36 na cup ni ukubwa wa matiti mfano D maana yake ukubwa wa band kifua chini ya matiti ni 36 nchi D ni ukubwa wa CUP ambapo namna yakupata ukuwa wa cup utaelezwa hapa chini:
Kuwa na kipimio (Tape measure) kwanza pima ukubwa wa bust (kipimo kipite chini ye matiti) hakikisha kipimo kinagusa pale matiti yanapo anzia, pitisha kipimo kuzunguka mgongo hadi pale ulipo anzia. Hakikisha kipimo kimeshika sawa sawa (kimenata) Kukuwa kipimo katika nchi (inches) Kama matokea ni namba shufwa (even) jumlisha 4 kama ni witiri (odd) ongeza 5 jumla yake intakuwa ni band size.
Halafu pima matiti kwa ujumla; pitisha kipimo juu ya matiti hakikisha kipimo kina pita usawa wa chuchu, kuzunguka mgongo - usibane wala usilegeze! Matokeo ya kipimo hiki ndiyo bust size.
Ili kupata cup size (kikombe cha sidiria) tutafanya mahesabu kidogo!!! Chukuwa Bust size toa Band size
1. Kama Bust size na Band size zina ukubwa sawa basi wewe ni saizi A
2. Kama bust ni kubwa zaidi ya band kwa takriban nchi 1 basi wewe ni size B
3. Nchi 2 zaidi wewe ni saizi C

Hebe tuangalie sasa mfano umepata 30 inchi hii ni namba shufwa ongeza 4 ili kupata bust ambayo ni band 34 halafu unapima matiti usawa wa chuchu kuzunguka mgongo unapata 36 inchi. 36-34 = 2 kwa vile ukubwa wa bust umezidi band kwa 2 basi wewe ni 34C kama ingekuwa imezidi kwa 2 na nusu basi wewe ni 34CC
NB kwa wale wenye matiti yaliyo anguka lazima uvae sidiria yoyote nyepesi itakayoshikilia matiti ili uweze kupata urahisi wa kupima bust.

Thursday 17 November 2011

Kukojowa kitandani

watoto hutofautiana sana katika uwezo wao wa kudhibiti vibofu vyao vya mkojo wakati wa usiku na wanaweza kukojoa kitandani bila wenyewe kujuwa. Watoto wengi huacha bedwetting wakiwa na umri kati ya miaka mitatu na miaka mitano, wengine wanaweza kuendelea hadi wakiwa wakubwa. Ina semakana mtu mmoja katika kila watu mia huendelea kukojowa wakiwa na miaka 18. Guess what wavulana ni wagumu kuacha kukojoa kitandani.Ingawa kibovu kinakua na kuwa imara kadri mtoto akuavyo lakini wakati mwingine mfumo wa misuli ya ufahamu – nervous system ambayo inahusika na ku control inachelewa kukuwa au mara nyingine mtoto anaweza kuwa wa usingizi mzito – heavy sleeper. Wakati mwingine tatizo hili husababishwa na bakteria katika kibofu. Shauku inaweza kuwa sababu pia mfano mtoto ameanza shule au ameanza kuogopa vitu mbali mbali katika dunia yake hiyo ndogo
Tiba: Kama tatizo halisababishwi na bakteria basi matibabu bora ni kutotumia dawa yeyote!!! Bali kumpa mtoto faraja na kuepuka kuumpa adhabu au kumwaibisha kwa wenzake kwani hatua hii itafanya tatizo liendelee na kwa kubwa zaidi, la maana ni kumpa zawadi pale anapokuwa hakukojoa kitandani. Jaribu kutumia tandiko lenye mpira maalumu wa kuzuina maji, hakikisha mtoto hanywi maji au jusi masaa kadhaa kabla ya kulala; anza na saa 1, 2, 3 nk . Mwisho jaribu mtoto eande haja kabla ya kulala.

Harufu ya kwapa

Harafu ya jasho inakera, kibaya zaidi ni kuwa wewe mwenyewe husikii harufu hiyo ila wale walio karibu yako. Kwa upande mwingine kujaribu kuzuia kutoka jasho ni hatari kwa afya yako na kujaribu kuondoa harufu kwa kutumia pafyumu husababisha madhara mengine ya kiafya na kwa bahati mbaya perfume zina jaribu poteza harufu kwa mda mfupi tu na sio kutokomeza tatizo hilo.
Dawa rahisi ya kuondoa harufu kwenye armpits yako ni kutunza mwili wako – kuoga mara kwa mara hata ikibidi mara tatu kwa siku kwa kuanzia! kwani harufu mbaya ya kwapa inatokana na kuwepo kwa bakteria katika kwapa hasa kukiwa na unyevu au maji maji kwapani.Ili kukomesha tatizo hili ni lazima kuoga mara nyingi wakati unaoga mkazo utiliwe kwenye kwapa tumia dodoki unaposafisha kwapa lako, pili ni lazima ukaushe kwapa barabara ili kuondoa unyevu ambao unakaribisha bakteria ambao wanajribu kuvunja vunja jasho lako na ndiyo maana linatoa harufu kali. Baada ya kuoga tumia potassium alum au sulphur.
Vile vile jitahidi kuepuka nguo za polista (polyster) vaa nguo za pamba 100% Punguza kula vyakula vyenye viungo vikali kama vitunguu swaumu nk.

Friday 4 November 2011

Karibu

Kujitengenezea mwenyewe (au DIY: Do It Yourself) ni neno linalotumika kueleza kubadilisha, au ukarabati wa vitu bila msaada wa wataalam au mafundi.
Katika miaka ya hivi karibuni. 
Jifanyie ( DIY) itahusisha harakati za Sanaa na Crafts, madawa asilia, Computer. Mtandao, simu za mikono michezo, mapishi nk  ili kukidhi mahitaji na kupunguza gharama zisizo za lazima. Tafadhali changia taaluma uliyo nayo ili wengine waweze kunufaika.