Pages

Thursday 25 October 2012

Vyakula muhimu vinavyoboresha Ngono

Vyakula muhimu vinavyosaidia kuleta nyege na kuboresha Ngono. Hivi ni baadhi tu kuna vingine pia. Tafadhali vyakula vingine sikuweza kupata tafsiri sahihi ya kiswahili. Kama unahitaji orodha zaidi comment.

1.     Cerery ni aina ya mboga mboga (mmea) ambao ni chanzo mwafaka cha kusisimua ngono, hii ni kwa sababu mmea huu unatengeneza homoni za androsterone homoni itolewayo kupia jasho. Harufu ya jasho hilo humfanya mwanamke kujisikia nyege na kutaka kufanya tendo la ngono na mtu huyo. Imependekezwa kuliwa ikiwa mbichi.





2.     Oyster wabichi wamejaa zinki ambayo husababisha uwingi wa shahawa na testosteron kwenye mapumbu, oyster vile vile ni chemi chemi ya dopamine homoni ambayo husababisha nyege. Jaribu kulishana oyster kabla ya kitendo cha ngono.







3.     Ndizi (hasa ndizi mzuzu) ina enzemu ( enzyme ) za bromelain ambazo husaidia kuongeza nyege na kuhamasisha ulijari (kinyume cha uhanithi) Ndizi vile vile ni chanzo tajiri cha vitamini B na potasiamu ambazo huongeza nguvu za mwili.



4.     Mti wa avokado uliitwa mti wa mapumbu wa kati wa dola ya Kiaztec huko Amrerica ya kusini. Avokado ina kiwango cha juu cha folic asidi amayo husaidia kuimarisha usagaji wa chakula na kukupa nguvu ya mwili. Vile vile ina vtamini B6 ambyo huongeza homi za kiume na potasiamu ambayo husaidia kurekebisha thyrod glands kwa wanawake kitendo hiki husaidia kuongeza nyege kwa wanawake na wanaume.





5.     Almonds ni chanzo kikuu cha asidi za mafuta, mafuta haya ni malighafi ya uzalishaji wa homoni zenye afya, vile vile harufu ya almonds huwafanya wanawake kupandwa na nyege pale wanapo hisi harufu hiyo kwa hali hii mbali na kula almonds jaribu kuwasha mshumaa wenye marashi ya almond kupandisha mahanjamu ya mwanamke wako.




Vyakula vingine ni kama: Asparagus, chokoleti, figi, basil, vitunguu swaumu, magome ya Yohimbe, Tribulus pamoja na Maca (sikuweza kupata neno la kiswahili tafadhali toa tafsiri kama unayo)

6.   Asparagus




7.   Chokoleti



Chokoleti huongeza msukumo wa damu kwenye uume na uke, ina L-arginine, amino acid ambayo ni nyenzo asilia ya kuhamasisha ngono  kwa wanawake na wanaume. Hufanya kazi kwa kuongeza oksidi ya nitriki na kukuza damu kati yake na viungo vya ngono, ambayo huongeza hisia, kuridhika, na nyege. Unashauriwa kula chokoleti nyeusi ambayo haijaongezwa sukari, pipi, karanga na au vikorombwezo vingine.


8.   Figi



Kula Figi ghafi kunaweza kufanya maajabu kwa afya yako ya uzazi na stamina ya ngono lakini kupikia na maziwa kutaongeza uwezo wake kwa kiasi kikubwa. Au unaweza kula figi pamoja na kunywa maziwa kabla ya kulala mfululizo kwa kipindi cha mwezi, matokeo yatakufanya uwe bora katika kujamiiana.

9.   Vitunguu swaumu



 
 

Saturday 28 January 2012

Kusafisha pasi yenye mgando mwesi

Wengi wetu tumesha tokewa na tatizo la kuunguza nguo na kusababisha mgando wa namna fulani hivi kwenye pasi. Hasa hasa nguo za polista kwani nguo za pamba 100% hazina matatizo haya. Jinsi unavyo zidi kutumia pasi hiyo ndivyo uchafu chini ya pasi unavyo zidi kujaa na kufanya upigaji pasi kuwa mgumu. Thank god tatizo hilo si tatitizo tena kwani nina njia moja rahisi sana wala haigharimu hata senti tano.
Vifaa:
1. Pande moja la mkaa

Njia:
Chukuwa kipande cha mkaa; ukubwa utachangia uharaka kwani utasafisha eno kubwa na kufanya kazi hiyo kumalizika haraka. Ili kufanikiwa haraka lazima mkaa huo uwe ulisha tumika jikoni na kupoa (Uliozimika)siyo ule uliozimwa kwa maji. Ili kuzima mkaa vizuri itabidi uufunike na chombo kukibwa kama sufuria nk kwani mkaa ukikosa oksijeni huzimika taratibu!!!!!!
Washa pasi yako kama niya umeme, kama niya mkaa basi ipashe moto iwe na joto fulani hivi. Kumbuka jinsi pasi inavyokuwa na umoto rahisi inakuwa kuisafisha! Chukuwa kipande hicho cha mkaa sugua eneo la pasi lililozingirwa na uchafu (mgando mweusi)
Endelea kusugua hadi utakapo ridhika.