Pages

Thursday 27 June 2013

Hesabu za Haraka za Wajanja


Wengi wetu tumezoea njia ndefu za kuzidisha. Hii njia ni moja tu kati ya nyingi kuwasaidia wale ambao kidogo hesabu za haraka haraka inakuwa jambo! Hii njia ina vipengele viwili vya kuzingatia.
Mfano wa kwanza:

13X12 : jumlisha 2 na 13 = 15
              zidisha 2  kwa 3 =   6 weka hii 6 mbele ya 15 utapata 156
Kwa kuwa tumezidisha 2x3na jibu halijazidi 10 (base of 10) hakuna mlolongo!




Mfano wa pili
Mfano huu namba itakayo zidishwa itazidi 10 (base of ten) kwa hiyo tuta fuata mkondo tofauti kidogo.

14X17 : jumlisha 7 na 14 = 21
             zidisha 7 kwa 4  = 28 weka 8 mbele ya 21 halafu 2 (hiyo ya njano) juu ya 1 (hivyo moja ya 21) utapata 238





Wednesday 26 June 2013

Zijuwe namba za viatu kimataifa

Kutambua namba ya viatu vyako kutawezesha kuburudika, kutembea kwa muda mrefu bila kuchoka au maumivu.
viatu vinavyobana huleta maumivu mna matatizo mengine ya miguu
Viatu ambavyo ni vikubwa husababisha malengelenge na kukufanya ubadilishe mwendo wako 
Usidhani kwamba ukubwa wa miguu yako wa sasa ni sawa na ule wa zamani, ukubwa wa miguu hubadilika mara kwa mara.
Namna ya kupima miguu yako:
Jipime wakati wa jioni wakati miguu yako imefura 
wakati wa kupima vaa soksi ambazo unategemea kuvalia viatu hivyo
Pima miguu yote na chagua vipimo vya mguu mkubwa
kama unajipima mwenyewe basi kaa kitini ili kupata vipimo halisi na kwa urahisi; usisimame!
unaweza kupima kwa kutumia inch au sentimeta, kisha zidisha inch mara 2.54 ili kupata sentimeta.

Unapima vipi



Wakati umekaa ganyaga kipande cha karatasi, tumia kalumu kuchora mguu wako ikiwa ime nyooka.
Kipimo utachopata toa milimeta 5 au 1/5 ya inch matokeo ndiyo yatakayo amua namba ya viatu vyako.


WANAUME
InchICMUSAEUROPEUK 
9.25"23.56395.5
9.5"24.16.5396
9.625"24.47406.5
9.75"24.87.540-417
9.9375"25.48417.5
10.125"25.78.541-428
10.25"269428.5
10.4375"26.79.542-439
10.5625"2710439.5
10.75"27.310.543-4410
10.9375"27.9114410.5
11.125"28.311.544-4511
11.25"28.6124511.5
11.5625"29.4134612.5
11.875"30.2144713.5
12.1875"31154814.5
12.5"31.8164915.5


WANAWAKE
InchICMUSAEUROPEUK 
8.1875"20.84352
8.375"21.34.5352.5
8.5"21.6535-363
8.75"22.25.5363.5
8.875"22.5636-374
9.0625"236.5374.5
9.25"23.5737-385
9.375"23.87.5385.5
9.5"24.1838-396
9.6875"24.68.5396.5
9.875"25.1939-407
10"25.49.5407.5
10.1875"25.91040-418
10.3125"26.210.5418.5
10.5"26.71141-429
10.6875"27.111.5429.5
10.875"27.61242-4310








Tuesday 25 June 2013

Namna ya kufunga Tai

Kwa wale wanaopenda kujinyonga basi namna yake ni hii hapa .




Vinginevyo jaribu kuangalia video hii hapa chini.






Thursday 25 October 2012

Vyakula muhimu vinavyoboresha Ngono

Vyakula muhimu vinavyosaidia kuleta nyege na kuboresha Ngono. Hivi ni baadhi tu kuna vingine pia. Tafadhali vyakula vingine sikuweza kupata tafsiri sahihi ya kiswahili. Kama unahitaji orodha zaidi comment.

1.     Cerery ni aina ya mboga mboga (mmea) ambao ni chanzo mwafaka cha kusisimua ngono, hii ni kwa sababu mmea huu unatengeneza homoni za androsterone homoni itolewayo kupia jasho. Harufu ya jasho hilo humfanya mwanamke kujisikia nyege na kutaka kufanya tendo la ngono na mtu huyo. Imependekezwa kuliwa ikiwa mbichi.





2.     Oyster wabichi wamejaa zinki ambayo husababisha uwingi wa shahawa na testosteron kwenye mapumbu, oyster vile vile ni chemi chemi ya dopamine homoni ambayo husababisha nyege. Jaribu kulishana oyster kabla ya kitendo cha ngono.







3.     Ndizi (hasa ndizi mzuzu) ina enzemu ( enzyme ) za bromelain ambazo husaidia kuongeza nyege na kuhamasisha ulijari (kinyume cha uhanithi) Ndizi vile vile ni chanzo tajiri cha vitamini B na potasiamu ambazo huongeza nguvu za mwili.



4.     Mti wa avokado uliitwa mti wa mapumbu wa kati wa dola ya Kiaztec huko Amrerica ya kusini. Avokado ina kiwango cha juu cha folic asidi amayo husaidia kuimarisha usagaji wa chakula na kukupa nguvu ya mwili. Vile vile ina vtamini B6 ambyo huongeza homi za kiume na potasiamu ambayo husaidia kurekebisha thyrod glands kwa wanawake kitendo hiki husaidia kuongeza nyege kwa wanawake na wanaume.





5.     Almonds ni chanzo kikuu cha asidi za mafuta, mafuta haya ni malighafi ya uzalishaji wa homoni zenye afya, vile vile harufu ya almonds huwafanya wanawake kupandwa na nyege pale wanapo hisi harufu hiyo kwa hali hii mbali na kula almonds jaribu kuwasha mshumaa wenye marashi ya almond kupandisha mahanjamu ya mwanamke wako.




Vyakula vingine ni kama: Asparagus, chokoleti, figi, basil, vitunguu swaumu, magome ya Yohimbe, Tribulus pamoja na Maca (sikuweza kupata neno la kiswahili tafadhali toa tafsiri kama unayo)

6.   Asparagus




7.   Chokoleti



Chokoleti huongeza msukumo wa damu kwenye uume na uke, ina L-arginine, amino acid ambayo ni nyenzo asilia ya kuhamasisha ngono  kwa wanawake na wanaume. Hufanya kazi kwa kuongeza oksidi ya nitriki na kukuza damu kati yake na viungo vya ngono, ambayo huongeza hisia, kuridhika, na nyege. Unashauriwa kula chokoleti nyeusi ambayo haijaongezwa sukari, pipi, karanga na au vikorombwezo vingine.


8.   Figi



Kula Figi ghafi kunaweza kufanya maajabu kwa afya yako ya uzazi na stamina ya ngono lakini kupikia na maziwa kutaongeza uwezo wake kwa kiasi kikubwa. Au unaweza kula figi pamoja na kunywa maziwa kabla ya kulala mfululizo kwa kipindi cha mwezi, matokeo yatakufanya uwe bora katika kujamiiana.

9.   Vitunguu swaumu



 
 

Saturday 28 January 2012

Kusafisha pasi yenye mgando mwesi

Wengi wetu tumesha tokewa na tatizo la kuunguza nguo na kusababisha mgando wa namna fulani hivi kwenye pasi. Hasa hasa nguo za polista kwani nguo za pamba 100% hazina matatizo haya. Jinsi unavyo zidi kutumia pasi hiyo ndivyo uchafu chini ya pasi unavyo zidi kujaa na kufanya upigaji pasi kuwa mgumu. Thank god tatizo hilo si tatitizo tena kwani nina njia moja rahisi sana wala haigharimu hata senti tano.
Vifaa:
1. Pande moja la mkaa

Njia:
Chukuwa kipande cha mkaa; ukubwa utachangia uharaka kwani utasafisha eno kubwa na kufanya kazi hiyo kumalizika haraka. Ili kufanikiwa haraka lazima mkaa huo uwe ulisha tumika jikoni na kupoa (Uliozimika)siyo ule uliozimwa kwa maji. Ili kuzima mkaa vizuri itabidi uufunike na chombo kukibwa kama sufuria nk kwani mkaa ukikosa oksijeni huzimika taratibu!!!!!!
Washa pasi yako kama niya umeme, kama niya mkaa basi ipashe moto iwe na joto fulani hivi. Kumbuka jinsi pasi inavyokuwa na umoto rahisi inakuwa kuisafisha! Chukuwa kipande hicho cha mkaa sugua eneo la pasi lililozingirwa na uchafu (mgando mweusi)
Endelea kusugua hadi utakapo ridhika.

Saturday 19 November 2011

Shambulio la nyuki/manyigu

Nyuki ni tisho kubwa kwa watu ambao ni lazima wafanye kazi nje: wakulima, wafanyakazi wa ujenzi, askari wa doria, na hata wacheza mpira au teseme kila mtu, Nyuki huwa wakali wanapo chokozwa na hwachagui ni nani aliye wachokoza. Nyuki aliye kasirika utamsikia sauti yake ya kuzuzizima na mara nyingi huja kichwani na usoni. Ukiwa katika hali hii jaribu kujikinga kwa kujifunika uso hasa kwa kupandisha shati lako… sorry kwa kina dada!. Vinginevyo kimbia; mwendo kasi wa nyuki unakadiriwa kuwa 19-24km kwa saa hivi ni rahisi kumshinda.
  • Usijaribu kuwapunga kwa kitabu, kitambaa au kitu chochote kufanya hivyo ni kuwapambisha moto
  • Usikimbilie ndani ya mto ziwa, bwawa au pool
  • Usijikinge uso wako kwa mikono kwani haisaidii
  • Kimbia kwa muundo wa zig-zag
  • Kama upo karibu ya nyumba au gari ingia haraka
Baada ya kurupushani hii na matokeo yake umeumwa basi fanya ifuatavyo:
  •  Ondoa ‘mkuki wa nyuki’ kwa kutumia kucha credit card au kisu
  • Usijikune
  • Jipake siki pale ulipoumwa kwa kutumia pamba au kitambaa safi ; kumbuka sumu ya nyuki ni acid kwa hiyo tumia alkaline kusawazisha sumu ya manyigu ni alikaline tumia acid kusawazisha
  • paka papai, kitunguu, kitunguu swaumu pale ulipo umwa ili kupunguza uvimbe.














Friday 18 November 2011

Hangover

Kwa kifupi pombe ni sumu. Wakati unaingiza sumu mwilini mwako, mwili utapatwa na mtiso uliosababishwa na pomba kam matokeo ya sumu hiyo kutembea mwilini mwako. Hangover ni neno mwavuli ambalo linajaribu kukueleza kitu gani umeufanyia mwili huo. Mara kwa mara dalili ni pamoja na maumivu ya kichwa uchovu, na upungufu wa maji mwilini.

OK kabla ya ‘kuyatimba maji’ zingatia:
☺ Kula hasa chakula chenye mafuta kama nyama nk
☺ Kunywa maziwa
☺ Kunywa vijiko 2 vya mafuta ya olive
☺ Meza vidonge vya vitamin
☺ Jihari usichanganye pombe


Tiba:
Dawa ya kwanza kama unafanya kazi piga simu kazini kwako na uwaambie boss kuwa unaharisha sana na kasha pata usingizi wa kutosha.
Mara tu utakapoamka pata glass mbili za maji baridi kasha kikombe kidogo cha kahawa kwa kuwa kahawa inasaidia kurudisha mishipi ya damu iliyovimba katika hali yake ya kaida jihadhari usinywe.
Kunywa juisi ya kutosha hasa juisi ya madaransi, nyanya au machungwa glasi kubwa inatosha
Jihadhari na kunywa kahawa kwa sababu caffeine siyo mzuri kwa hali hiyo
Kunywa KUDZU ni dawa ya kienyeji ya Kichina kama kifungua kinywa. Kinywaji hiki kinaweza kupatikana katika maduka ya chakula kwa afya.
Ukipata nafuu kunywa supu hasa ya kuku itasaidia kurudisha potassium uliyopoteza.
Milkshake ya ndizi; changanya nusu kikombe cha maziwa ndizi mbivu pamoja na asali vijiko vya chai 2.