Pages

Thursday, 27 June 2013

Hesabu za Haraka za Wajanja


Wengi wetu tumezoea njia ndefu za kuzidisha. Hii njia ni moja tu kati ya nyingi kuwasaidia wale ambao kidogo hesabu za haraka haraka inakuwa jambo! Hii njia ina vipengele viwili vya kuzingatia.
Mfano wa kwanza:

13X12 : jumlisha 2 na 13 = 15
              zidisha 2  kwa 3 =   6 weka hii 6 mbele ya 15 utapata 156
Kwa kuwa tumezidisha 2x3na jibu halijazidi 10 (base of 10) hakuna mlolongo!




Mfano wa pili
Mfano huu namba itakayo zidishwa itazidi 10 (base of ten) kwa hiyo tuta fuata mkondo tofauti kidogo.

14X17 : jumlisha 7 na 14 = 21
             zidisha 7 kwa 4  = 28 weka 8 mbele ya 21 halafu 2 (hiyo ya njano) juu ya 1 (hivyo moja ya 21) utapata 238





No comments:

Post a Comment